humph the GREAT
Mkongwe kutoka unyamani TID amezitaka kampuni mbali mbali kutangaza na wasanii wakongwe kwa kuwa wao ndio mizizi iliyohangaika kuisimamisha misingi ya bongo fleva mpaka kuanza kuheshimiwa na makundi ya rika zote.
Mkongwe TID

Akizungumza
na Planet Bongo ya East Africa Radio kuhusu heshima ya Bongo fleva kwa
wakongwe, TID amesema wakongwe wengi hawapatiwi 'deal' za matangazo kama
wasanii wa sasa ambao wengine wamekuwa wakionesha dharau bila kujua
gharama waliyotumia kusimamisha heshima ya muziki.
"Makampuni yanayotoa hizi
deal kwa wasanii wa sasa wanakosea kwa sababu wanatoa kazi mbaya na
hawana vitu vya maana kama sisi wakongwe . Sisi pia tuna kazi nzuri
ambazo zinaweza kuuza na pia tuna tambua jamii inataka nini ndiyo maana
tulihangaika kutengeneza msingi mzuri wa muziki" TID alifunguka.
Tags
Michezo na burudani