humph the GREAT
"Katika mwaka wa fedha 2016/17 jumla ya watumishi wa Umma 90721
wamekwisha ajiriwa kwa kuzingatia vipaumbele na mahitaji ya kila mwajiri
na katika mwaka wa fedha 2017/18 serikali inatarajia kuajiri watumishi
52436 wa sekta mbalimbali kwa kuzingatia vipaumbele vya taifa pamoja na
kuimarisha kila sekta na upungufu mkubwa wa watumishi wa Umma" -alisema
Kairuki
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki
amefunguka na kusema serikali kwa sasa haitaweza kuajiri walimu wapya wa
sanaa bali itawatumia walimu wa sanaa wa ziada waliopo katika shule za
sekondari.
Angela Kairuki amesema hayo leo bungeni na kudai kila shule itaweza kupata walimu wa sanaa kulingana na mahitaji yao
"Utafiti uliofanywa na Ofisi ya Rais Tamisemi mwaka 2015/2016 umebaini
kuwepo kwa ziada ya walimu wa masomo ya sanaa wapatao 7463 katika shule
za sekondari, kutokana na hali hii serikali inaendelea na zoezi la
kuwagawanya walimu hao au kuwa 'redeploy' kwa kuzingatia uwiano na
mahitaji halisi ya walimu wa sanaa kwa kila mamlaka za serikali za mitaa
ili kila shule iweze kupata walimu wa masomo ya sanaa badala ya kuajiri
walimu wapya" -alisema Angela Kairuki
Mbali na hilo Waziri Kairuki amesema serikali inaendelea kuajiri
watumishi wa kada mbalimbali ambapo katika mwaka wa fedha 2016/2017
watumishi zaidi ya elfu tisa wameajiriwa serikalini.
Tags
HABARI
