humph the GREAT
MTANGAZAJI wa kipindi cha Harusini kinachorushwa kupitia Magic Swahili, Pennieli Mungwila ‘Penny’ amefungukia vazi la harusi alilovaa na kuwaacha watu kwenye sintofahamu kuwa hajaolewa na kwamba nafasi bado iko wazi.
Akizungumza na Star Mix, Penny alisema kuwa, gauni alilovaa ni kwa ajili tu ya kurekodi kipindi chake na sio kwamba ilikuwa ni harusi yake ya ukweli kama watu wengi walivyodhani.
“Jamani nisije kukosa mume bure, gauni lile nilivaa kwa ajili ya kazi tu na si kwamba nilikuwa naolewa kweli kama watu walivyodhani,” alisema Penny.
Akizungumza na blog hii, Penny alisema mwaka huu yuko tayari kwa ndoa na kwa mwanaume sahihi kwani ameomba vya kutosha.
“Mwaka huu ni wa baraka kwangu na gundu nyingi zimeshaondoka 2017, mwaka huu kwangu ishallah shela litakaa mwilini mwangu, mwanaume yupo tayari,” alisema Penny bila kumtaja jina mwanaume wake.

Tags
Udaku