Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Ticker

6/recent/ticker-posts

Morison awafarakanisha watani

humph the GREAT
UONGOZI wa klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam,  umepeleka rasmi malalamiko Shirikisho la Soka nchini (TFF) dhidi ya Klabu ya Simba ya Dar es Salaam pia ikidai inamshawishi winga wake, Bernard Morrison,  kujiunga na klabu hiyo kinyume cha sheria na ikitaka haki itendeke na hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Wakili Simon Patrick,  amesema klabu haiwezi kufumbia macho maelezo yaliyotolewa na winga huyo ambaye ameweka wazi kila kilichotokea.

“Mchezaji wetu ameeleza kila kitu, hivyo tumepeleka malalamiko yetu TFF na chombo husika kitayasikiliza kutokana na ushahidi tuliouwasilisha na kuutolea maamuzi,” amesema Patrick na kuongeza kwamba tayari ushahidi umekusanywa kwa ajili ya suala hilo ikiwa ni pamoja na kumhoji mchezaji na vielelezo vingine vinavyohusiana na suala hilo.

Source:Yanga App.

Post a Comment

0 Comments