humph the GREAT
UONGOZI wa Klabu ya Simba umemuweka sokoni kiungo mshambuliaji wake, Shiza Kichuya kwa kukaribisha ofa kutoka klabu yoyote.
Hivi karibuni Klabu ya Ismailia ya
Misri ilishindwana na Simba juu ya dau la kumuuza kiungo huyo ambalo
lilikuwa dogo, hivyo kusababisha uongozi wa klabu hiyo kukataa.
Kichuya ni miongoni mwa wachezaji wa
Simba ambao wanacheza kwa kiwango kizuri na kuisaidia timu yake hiyo,
jambo ambalo timu nyingi zimekuwa zikimnyemelea.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara,
amefunguka kuwa, dili lao na Ismailia juu ya kumchukua Kichuya limekufa
rasmi, lakini wamemuweka sokoni mchezaji huyo kwa timu yoyote
itakayomhitaji.
“Ile dili kati yetu na Ismailia
ilishakufa rasmi kwa sasa hakuna ishu ya Kichuya kwenda huko, lakini
tupo tayari kupokea ofa yoyote ile, iwapo kuna timu itamhitaji tutakuwa
tayari kumuuza mchezaji huyo.
“Simba tumekuwa na desturi ya kuwaachia
wachezaji wetu kuwauza pale tunapofanikiwa kupata timu ya kucheza,
hivyo mchezaji yeyote yule atakayetakiwa tutakuwa tayari kumuachia,” alisema Manara.
Khadija Mngwai, Dar es Salaam.
0 Comments